WHO yatangaza dawa mpya za kupambana na ukimwi .

SHIRIKA la Afya Ulimwenguni (WHO),
limetangaza kuwa matumizi ya dawa
tatu za aina tofauti za kuzuia makali ya
Ukimwi (ARVs) kwa watu wanaoishi na
virusi vya ugonjwa huo, ni kati ya
kinga muhimu za kupambana na
maambukizi.
Kulingana na ripoti ya shirika hilo
iliyotolewa hivi karibuni,
mchanganyiko huo wa tiba uliopewa
jina la ufupisho wa maneno ART
unafanya kazi bora zaidi kuliko
matumizi ya dawa moja moja ya ARVs.
Katika mfumo wa matumizi ya ARVs
uliopo sasa, mgonjwa hutumia aina
moja ya dawa katika  maisha yake yote
ili kuzuia virusi.
Tangazo la WHO, limesema kama
mmoja wa wanandoa, ana virusi na
mwingine hana, matumizi ya ART kwa
muathirika ni muhimu kama ilivyo
katika kutumia kondom.
Tangazo hilo limesema hiyo inatokana
na utafiti uliobaini kuwa baada ya
matumizi ya ART kwa muda fulani,
mtu anayeishi na virusi, anakuwa
hawezi kumwabukiza mtu anayefanya
naye tendo la ndoa.
Ingawa ripoti ya utafiti huo
haikufafanua kwa kina ni kwa kiasi gani
mtu anapaswa kutumia ART,
inashauriwa kuwa kabla ya mtu
kutumia dawa, lazima kwanza
ashauriwe na daktari.
Katika taarifa yake yenye kurasa 54 ya
Aprili mwaka huu yenye namba ISBN
978 92 4 150,197 2, WHO pia
imesisitiza umuhimu wa watu kupima
afya zao.
Shirika hilo lisema kwa sasa ni asilimia
40 tu ya watu wenye virusi duniani
ndio waliowahi kwenda hospitalini na
kupima afya zao ili kujua nafasi zao
katika ugonjwa huo.
Kwa mujibu wa shirika hilo, kiwango
hicho ni kidogo mno.
Aidha wanandoa ni asilimia 50 ya
watu wote wenye virusi ambao
baadhi yao mmoja ana virusi,
mwingine hana, hali ambayo ni hatari
zaidi ikiwa hawatajua nafasi za afya
zao na kuchukua tahadhari.
“ART hupunguza ongezeko la virusi
vya Ukimwi mwilini. Mtu akitumia
dawa hiyo, anajihisi mwenye afya
njema kwa muda mrefu zaidi,
inasema sehemu ya taarifa ya shirika
hilo.
Kutumia na kuacha, au kutumia aina
fulani na kuacha nyingine huzuia
uwezo wa dawa za ART kufanya kazi,
kwa maana hiyo ni suala la msingi
kabla ya kufanya chochote kupata
ushauri wa daktari,” ilisisitiza taarifa.

Advertisements

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s