Thamani ya umuhimu wa tunda avocado au parachichi

PARACHICHI

(AVOCADO)
Ndani ya tunda hili kuna maji
kiasi kidogo sana
ukilinganisha na matunda
mengine lakini kuna mafuta
mengi na unaweza
kuchanganya kula na tunda
lingine kama vile apple, ndizi,
chungwa au hata maziwa
kwa kutengeneza juisi.
TINDIKALI
Licha ya kuwa na mafuta
parachichi lina tindikali (acid)
mbalimbali ikiwemo
inayojulikana kama amino
ambayo husaidia sana
kukinga na kutibu maradhi
katika mwili wa binadamu.
Tunda hili pia lina protini ya
kiwango cha juu.
Pia kuna tindikali inayoitwa
oleic acid kwenye parachichi
ambayo husaidia kukinga
magonjwa ya moyo, kiharusi
na kansa.
VITAMINI “E” NA B6
Imeelezwa na wataalamu
kuwa tunda hili lina kiwango
kikubwa cha vitamini E kuliko
ile inayopatikana kutoka
kwenye mazao ya
wanyama.Parachichi lina
vitamini hiyo nyingi kuliko
inayopatikana katika mayai
ambayo yanasifika kwa kuwa
na vitamini e, hivyo hii
inathibitisha kuwa lina faida
kubwa mwilini.
Licha ya vitamini E pia ndani
ya parachichi kuna vitamini
B6 na kuna madini ya
chuma (Iron) kwa wingi na
madini ya potassium,
pamoja na vitamin B6 na E
mlaji anaweza kuletawa
nafuu sana kama alikuwa na
matatizo ya stress, matatizo
ya uzazi kama ugumba na
jogoo kutopanda mtungi
Nguvu za kiume pia tunda
hili linasaidia (impotence) .
FAIDA ZA PARACHICHI
Licha ya binadamu kufaidika
na virutubisho vya tunda hili
kuna faida nyingi za
parachichi kama vile majani
ya mti wake pamoja na
magamba, baadhi ya watu
hutumia kutibu maradhi ya
kuharisha.
Majani na magamba hayo
hutibu pia tatizo la gesi
tumboni, kutuliza kikohozi
pamoja na matatizo ya ini na
kusafisha njia ya mkojo.
Hata hivyo, kwa mujibu wa
wataalamu wa dawa za
mitishamba, dawa hii haifai
kutumiwa na wanawake
ambao wana mimba kwani
wakitumia inaweza
kusababisha kuharibika kwa
ujauzito.
HEDHI
Hata hivyo, wataalamu wa
tiba mbadala wanasema
dawa hiyo inaweza
kuwasaidia sana wanawake
ambao wameshindwa kuona
siku zao kwa wakati, na
wakitumia vyema wanaweza
kuanza kuona siku zao .
Aidha, tunda hili linasaidia
uyeyushaji wa chakula
tumboni hasa kwa wale
wenye matatizo ya vidonda
vya tumbo, kwani parachichi
lina nyuzinyuzi “fiber”
ambayo ni muhimu kukinga
kuta za utumbo. Watu wenye
maradhi ya anaemia,
diabetes, matatizo ya mfumo
wa neva, matatizo ya
mishipa ya moyo hasa wa
artery wanashauriwa kula
tunda hili mara nyingi.
Lakini pia tunda hili
limethibitishwa na
wataalamu kuwa
linapunguza kwa kiwango
kikubwa cholesterol kutoka
kwenye damu hasa kwa watu
wanene.
Tunda hili husaidia
kulainisha ngozi na kuondoa
mikunjo, hung`arisha na
kulainisha nywele na
kuzisaidia kukua pia
kuziimarisha na kuzuia
kukatikakatika.
Parachichi unaweza kulila
kwa kulimenya au kwa
kulisaga na kutengeneza juisi
na kama nilivyoeleza hapo
juu unaweza kuchanganya
na matunda mengine kama
tulivyoyataja na hutaharibu
virutubisho vilivyomo badala
yake utaongeza ubora wa
juisi yako.
Watoto wadogo pia unaweza
kuwapa tunda hili na
wakafaidika na haya
tuliyoyaandika.
Parachichi pia huweza
kutumika kama siagi kwa
kupaka kwenye mkate au
kuchanganya na wali.
Haya wale wanaopenda ngozi zao
za mwilini zisijikunje hata wakiwa
watu wazima wadumu kula tunda
hili kila siku katika maisha yao basi
ngozi za mwili wao hazitajikunja
hata usoni watakuwa kila siku vijana
hata wakiwa wazee.

Advertisements

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s